Duration 2:27

UJASILIAMALI KUSAGA KARANGA

11 141 watched
0
31
Published 8 Feb 2016

KWA kuiga tamaduni za watu wa magharibi bila kujadili kuhusu suala la mazingira, jiografia, uchumi, changamoto za kipato cha mtu mmoja mmoja na mfumo wa elimu yetu, siyo siri tutabaki kulaumu vijana wa leo kukosa ajira, siyo kwa wasio na elimu tu bali hata wale wanaotoka vyuoni kwani hawakuandaliwa kujiajiri na hawana moyo wa kujituma wala hawajui wapi pa kuanzia linapokuja suala la kujiajiri.. Kamera yangu iliwanasa watoto hawa katika soko la jioni la Pasiansi wilayani Ilemela jijini Mwanza. Kwa mujibu wa mazungumzo niliyofanya nao wanasema mara baada ya masomo nyakati za jioni hushiriki zoezi hili la kuwasaidia wazazi wao, zaidi ni mama zao katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali wa kusaga karanga za wateja wanaofika sokoni hapo. Wateja wanaponunua karanga toka sokoni, karanga hizo hukaangwa na mama wa watoto hawa kisha watoto kushiriki zoezi la kuwasaidia mama zao kusaga karanga hizo kwa kutumia nyenzo hii ya kurahisisha usagaji karanga kama sehemu ya biashara. Mama ndiye mpokea pesa, ambayo hutumika kwenye kusukuma maisha ya kila siku.

Category

Show more

Comments - 1